Translations of Swahili Hymns
October 20, 2019 | By Vienna Scott, BF ‘21. Vienna is majoring in Religious Studies and Political Science.
For the reader's edification in meditation and appreciation of Swahili culture and language.
Stand Up and Fight (Make War)
Stand up and make war, soldiers of Christ
Raise the flag of his victory
He leads his forces here
All the enemies also, the Lord overcomes them
Hear the trumpet, calling us!
Let’s move forward, the goal is to win!
We should not be afraid, dangers of war
Fight the enemy, by the power of God!
Stand up and fight, in the name of Jesus!
It is good for us all to depend on him
And first let’s put on the armor of God
Let us always watch, pray earnestly!
Our contest here, it will end quickly
Then we will rest, after the war/battle
And every winner, he will receive a crown,
And much glory, near God
Simama Fanya Vita
1. Simama Fanya vita, askari wa Yesu!
Tuinue bendera ya ushindi wake!
Yeye huyaongoza, majeshi yake huku
Adui wote pia, Bwana awashinda.
2. Sikia baragumu, linalotuita!
Tuendelee mbele, lengo ni kushinda!
Tusiogope kamwe, hatari za vitani,
Pigana na adui, kwa nguvu za Mungu!
3. Simama fanya vita, kwa jina la Yesu!
Yafaa sisi sote, kumtegemea.
Na kwanza tuzivae, silaha zake Mungu!
Tukeshe siku zote, tuombe kwa bidi!
4. Shindano letu hapa, hima litakwisha,
Ndipo tutapumzika, baada ya vita.
Na kila mshindaji, atapokea taji,
Na utukufu mwingi, karibu na Mungu.
I am thirsty
I am caught with thirst (I thirst), Lord, please give me water
Water of life in my life
Lord, Lord, Jesus my King!
My heart loves you, Lord
My God. when will I come to you
Lord my King?
Afternoon and night Lord I will cry for you. People
say: “ Where is your God?”
Sorrow in my heart, Lord my God
Many people full of hatred, God forgive them!
We cling to each other to go up to heaven
We are thankful, we are happy to cooperate
Savior, why am I running short of strength in my heart
Help me Lord, I will thank you.
Ninashikwa na Kiu
1. Ninashikwa na kiu, Bwana, unipe maji,
Maji ya uhai ndani ya Maisha yangu.
:/: Bwana, Bwana, Yesu Mfalme wangu!
2. Moyo wangu wakupenda, Bwana
Mungu wangu. Nitakuja lini kwako,
Bwana Mfalme wangu?
3. Mchana na usiku Bwana nakulilia. Watu
Wanasema: “Mungu wako yuko wapi?”
4. Huzuni moyoni mwangu, Bwana Mungu wangu
Watu wengi wadharau, Mungu ‘wasamehe!
5. Twashikamana pamoja kwenda juu mbinguni.
Twashukuru, twafurahi kushirikiana.
6. Mwokozi, nguvu zaishaje moyoni mwangu?
Unisaidie Bwana, nitakushukuru.
It is a glorious day
it is a glorious day, hallelujah, amen
For rest, hallelujah, amen
we stop things to worship God
Lord in heaven, hallelujah amen
it is a glorious day, hallelujah, amen
Absolutely glorious, hallelujah amen
Come my brothers, we worship God
By spirit and truth, hallelujah, amen.
it is a glorious day, hallelujah, amen.
Of great joy, hallelujah, amen.
Jesus, risen and now alive
He is praying for us, hallelujah, amen.
it is a glorious day, hallelujah, amen.
Yes remarkable, hallelujah, amen.
We have a savior who saves us
Now and forever, hallelujah, amen.
it is a glorious day, hallelujah, amen.
Day of grace, hallelujah, amen.
Declare the word of the Lord Savior
Praise him always, hallelujah, amen.
Ni Siku Tukufu
1. Ni siku tukufu, haleluya, amina,
Ya kupum-zika, haleluya, amina.
Tuache shughuli tumwabudu Mungu,
Bwana wa mbinguni, haleluya amina.
2. Ni siku tukufu, haleluya, amina.
Tukufu kabisa, haleluya, amina.
Njoni ndugu zangu, tumwabudu Mungu,
Kwa roho na kweli, haleluya, amina.
3. Ni siku tukufu, haleluya, amina.
Ya furaha mno, haleluya, amina.
Yesu ‘kafufuka, na sasa yu hai,
Anatuombea, haleluya, amina.
4. Ni siku tukufu, haleluya, amina,
Ndiyo maarufu, haleluya, amina.
Tunaye Mwokozi atuokoaye,
Sasa na milele haleluya, amina.
5. Ni siku tukufu, haleluya, amina,
Siku ya neema, haleluya, amina.
Tangazeni Neno la Bwana Mwokozi,
Msifuni daima, haleluya, amina.